Posts

Showing posts from February, 2023

MASOMO YA MISA JUMAPILI, FEBRUARI 19, 2023

MASOMO YA MISA,FEBRUARI 19, 2023 Somo la Kwanza Law 19:1-2, 17-18 Bwana alinena na Musa, akamwambia, Nena na mkutano wote wa wana wa Israeli, uwaambie, Mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana, Mungu wenu, ni mtakatifu. Usimchukie ndugu yako moyoni mwako; ni lazima kumkemea jirani yako, wala usichukue dhambi kwa ajili yake. Usifanye kisasi, wala kuwa na kinyongo juu ya wana wa watu wako; bali umpende jirani yako kama nafsi yako; Mimi ndimi Bwana. Wimbo wa Katikati Zab 103:1-4, 8, 10, 12-13 Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana.  Naam, vyote vilivyo ndani yangu Vilihimidi jina lake takatifu.  Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana,  Wala usizisahau fadhili zake zote. (K) Bwana amejaa huruma na neema Akusamehe maovu yako yote,  Akuponya magonjwa yako yote,  Aukomboa uhai wako na kaburi,  Akutia taji ya fadhili na rehema,  (K) Bwana amejaa huruma na neema Bwana amejaa huruma na neema,  Haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhili. Hakututenda sawasawa na hatia zetu,...

MASOMO YA MISA, FEBRUARI 18, 2023

MASOMO YA MISA, FEBRUARI 18, 2023 Somo la Kwanza Ebr 11:1–7 Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana na mambo yasiyoonekana. Maana kwa hiyo wazee wetu walishuhudiwa. Kwa Imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri. Kwa Imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo, ijapokuwa amekufa, angali akinena. Kwa imanai Henoko alihamishwa, asije akaona mauti, wala hakuonekana, kwa sababu Mung alimhamisha: maana kabla ya kuhamishwa alikuwa ameshuhudiwa kwamba amempendeza Mungu. Lakini pasipo Imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao. Kwa imanai Nuhu akiisha kuonywa na Mungu katika habari za mambo yasiyoonekana bado, kwa jinsi alivyomcha Mungu, aliunda safina, apate kuokoa nyumba yake. Na hivyo akauhukumu makosa uli...

MASOMO YA MISA IJUMAA, FEBRUARI 17, 2023

MASOMO YA MISA, FEBRUARI 17, 2023 Somo la Kwanza Mwa 11:1–9 Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja. Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambarare katika nchi ya Shinari; ;wakakaa huko. Wakaambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala yam awe, na lami badala ya chokaa. Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilelel chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote. Bwana akashuka ili auone mji na mnara waliokuwa wakiujenga wanadamu. Bwana akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na hayo ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya. Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao. Basi Bwana akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji. Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo Bwana alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko Bwana a...

MASOMO YA MISA ALIAHAMISI, FEBRUARI 16, 2023

MASOMO YA MISA, FEBRUARI 16, 2023 Somo la Kwanza Mwa 9:1–13 Mungu akambariki Nuhu na wanawe, akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi. Kila mnyama nwa katika nchi atawaogopa ninyi na kuwahofu, na kila ndege wa angani; pamoja na vitu vyote vilivyojaa katika ardhi, na samaki wote wa baharini; vimetiwa mikononi mwenu. Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyoawapa mboga za majani, kadhalika nawapeni hivi vyote. Bali nyama pamoja na uhai, yaani, damu yake, msile. Hakika damu yenu ya uhai wenu nitaitaka; na kwa mkono wa kila mnyama nitaitaka; na kwa mkono wa mwanadamu, kwa mkono wa ndugu ya mtu nitataka uhai wa mwanadamu. Atakayemwaga damu ya mwanadamu, damu yake huyo itamwagwa na wanadamu; maana kwa mkono wake Mungu alimfanya mwanadamu. Nanyi zaeni, mkaongezeke; zaeni sana katika nchi, mkaongezeke ndani yake. Mungu akamwambia Nuhu, na wanawe pamoja naye, akisema, Mimi, tazama, nalithibitisha agano langu nanyi; tena na uzao wenu baada yenu; tena na kila kiumbe hai...

MASOMO YA MISA JUMATANO, FEBRUARI 15, 2023

MASOMO YA MISA JUMATANO, FEBRUARI 15, 2023 Somo la Kwanza Mwa 8:6–13, 20–22 Ikawa baada ya siku arobaini, Nuhu akalifungua dirisha la safina, alilolifanya; akatoa kunguru, naye akatoka akaenda huko na huko, hata maji yakakauka juu ya nchi. Kisha akatoa njiwa, aone kwamba maji yamepunguka usoni pa nchi; bali yule njiwa hakuona mahali pa kutua kwa wayo wa mguu wake, akamrudia Nuhu safinani, maana maji yalikuwa juu ya uso wa nchi yote; naye akanyosha mkono, akamtwaa, akamwingiza mle safinani. Akangoja na siku saba tena, akamtoa yule njiwa katika safina mara ya pili, njiwa akamjia jioni, na tazama, alikuwa na jani bichi la mzeituni kinywani mwake, ambalo amelitunda, basi Nuhu akajua ya kwamba maji yamepunguka juu ya nchi. Akangoja na siku saba tena, akamtoa yule njiwa; naye asimrudie tena kamwe. Ikawa mwaka wa mia sita na moja, mwezi wa kwanza, siku ya kwanza ya mwezi, maji yalikauka juu ya nchi. Nuhu akaondoa kifuniko cha safina, naye akaona, na tazama, uso wa nchi umekauka. Nuhu akamjeng...

MASOMO YA MISA JUMANNE, FEBRUARI 14, 2023

MASOMO YA MISA, FEBRUARI 14, 2023 Somo la Kwanza Mwa 6:5–8, 7:1–5, 10 Bwana akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analoliwaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote. Bwana akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo. Bwana akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya. Lakini Nuhu akapata neema machoni pa Bwana. Bwana akamwambia Nuhu, Ingia wewe na jamaa yako yote katika safina; kwa maana nimekuona wewe u mwenye haki mbele zangu katika kizazi hiki. Katika wanyama wote walio safi ujitwalie saba saba, mume na mke; na katika wanyama wasio safi wawili wawili, mume na mke. Tena katika ndege wa angani saba saba, mume na mke; ili kuhifadhi hai mbegu juu ya uso wa nchi yote. Kwa maana baada ya siku saba nitainyesha dunia mvua, siku arobaini mchana na usiku; na kila kilicho hai nilichokifanya juu ya uso wan chi nitakifutilia mba...

MASOMO YA MISA JUMATATU, FEBRUARI 13, 2023

MASOMO YA MISA, FEBRUARI 13, 2023 Somo la Kwanza Mwa 4:1-15, 25 Adamu alimjua Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, Nimepata mtoto mwanamume kwa Bwana. Akaongeza akamzaa ndugu yake, Habili. Habili alikuwa mchunga kondoo, na Kaini alikuwa mkulima ardhi. Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana. Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake; bali Kaini hakumakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana. Bwana akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana? Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyma dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde. Kaini akamwambia Habili nduguye, twende uwandani. Ikawa walipokuwapo uwandani, Kaini akamwinukia Habili nduguye, akamwua. Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu? Akasema,...

Taarifa kwa watumiaji

 Tumsifu Yesu Kristo. Tunapendanda kuwataarifu watumiaji wetu kuwa kutokana na maombi ya wengi ya kuwa  na masomo ya wiki nzima. Tutakuwa tunatuma masomo ya wiki nzima kila jumapili ya wiki. Asanteni Tunawatakia siku njema na Mungu awatunze