MASOMO YA MISA JUMAPILI, FEBRUARI 19, 2023
MASOMO YA MISA,FEBRUARI 19, 2023 Somo la Kwanza Law 19:1-2, 17-18 Bwana alinena na Musa, akamwambia, Nena na mkutano wote wa wana wa Israeli, uwaambie, Mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana, Mungu wenu, ni mtakatifu. Usimchukie ndugu yako moyoni mwako; ni lazima kumkemea jirani yako, wala usichukue dhambi kwa ajili yake. Usifanye kisasi, wala kuwa na kinyongo juu ya wana wa watu wako; bali umpende jirani yako kama nafsi yako; Mimi ndimi Bwana. Wimbo wa Katikati Zab 103:1-4, 8, 10, 12-13 Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Naam, vyote vilivyo ndani yangu Vilihimidi jina lake takatifu. Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana, Wala usizisahau fadhili zake zote. (K) Bwana amejaa huruma na neema Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote, Aukomboa uhai wako na kaburi, Akutia taji ya fadhili na rehema, (K) Bwana amejaa huruma na neema Bwana amejaa huruma na neema, Haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhili. Hakututenda sawasawa na hatia zetu,...